Kundi la wanasayansi mjini Vienna, Austria
wameanzisha mpango wa kuunda taifa la amani la
aina yake ambalo litakuwa na jina Asgardia.
Taifa hilo litaundwa katika anga za juu, eneo.
Maelezo kwenye tovuti ya wanasayansi hao
yanasema taifa hilo litakuwa nje ya udhibiti wa
mataifa yoyote ya sasa na litakuwa katika mzingo
wa dunia, eneo ambalo vyombo vya anga za juu
huzunguka dunia.
Wanasayansi hao wanapanga kurusha satelaiti ya
kwanza, ya kuanzisha taifa hilo, mwishoni mwa
mwaka ujao.
Mpango wa kupeleka watu wakaishi Mars
China yatuma wataalamu mzingo wa dunia
Matumaini ya wataalamu hao ni kwamba siku moja
hivi karibuni watatambuliwa na Umoja wa Mataifa.
Lakini baadhi ya wataalamu wanatilia shaka
uwezekano wa mpango huo kufanikiwa ikizingatiwa
kwamba sheria za kimataifa huzuia mataifa kudai
umiliki wa maeneo anga za juu.
"Raia" wa Asgardia, ambao watachunguzwa kwa
makini kabla ya kukubaliwa, mwishowe watapewa
hata pasipoti, anasema Lena de Winne, mmoja wa
maafisa wakuu wa mradi huo ambaye alifanya kazi
kwa miaka 15 katika Shirika la Anga za Juu la
Ulaya (EPA).
Mradi huo unaongozwa na shirika la Aerospace
International Research Center, ambalo lilianzishwa
na mwanasayansi Mrusi, ambaye pia ni
mfanyabiashara, Dkt Igor Ashurbeiyli.
Mashindano yanaandaliwa kuamua bendera na
wimbo wa taifa wa nchi hiyo mpya.
Profesa Sa'id Mosteshar, mkurugenzi wa Taasisi ya
Sera na Sheria za Anga za Juu ya London,
amesema itakuwa vigumu kwa Asgardia
kutambuliwa kama taifa ikizingatiwa kwamba
haitahusiana na taifa lolote linalojitawala duniani,
na pia 'raia wake' wengi watakuwa ardhini.
Tayari zaidi ya watu 50,000 wamewasilisha
maombi mtandaoni kutaka kuwa raia wa taifa hilo.j
No comments:
Post a Comment