Klabu ya soka ya Leicester City imeendeleza wimbi
la ushindi katika michuano ya ligi ya mabingwa
barani Ulaya baada ya kuibuka na ushindi wa bao
1-0 dhidi ya FC Copenhagen.
Wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani King
Power, Leicester walipata bao hilo dakika tano
kabla ya kwenda mapumzikoni kupitia kwa Riyad
Mahrez aliyekuwa katika kiwango cha hali ya juu
baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Mualgeria
mwenzake Islam Slimani.
Kwa matokeo hayo Leicester wanabaki kileleni
mwa kundi G wakiwa na alama 9 baada ya
kushinda michezo yote mitatu ya ufnguzi wa ligi
ya mabingwa Ulaya.
Timu pekee zilizowahi kushinda michezo mitatu ya
ufunguzi katika michuano hiyo ni AC Milan, Paris
St-Germain, Juventus na Malaga.
Matokeo mengine ya Ligi ya mabingwa barani
Ulaya
Bayer 04 Leverkusen 0-0 Tottenham Hotspur F.C.
CSKA Moscow 1-1 AS Monaco FC
Real Madrid 5-1 Legia Warsaw
Sporting 1 -2 Borussia Dortmund
Club Brugge 1-2 FC Porto
Dinamo Zagreb 0- 1 Sevilla
Lyon 0- 1 Juventus
No comments:
Post a Comment