Shirika la utangazaji la NBC nchini Marekani
limemfuta kazi mtangazaji Billy Bush ambaye
amekuwa akiendesha kipindi cha Today.
Mgombea urais wa chama cha Republican alikuwa
anahojiwa na Bw Bush miaka kumi iliyopita
alipotoa matamshi ya kudhalilisha kuhusu
wanawake.
Ukanda wa mahojiano hayo yaliyofanyika mwaka
2005 ulifichuliwa majuzi na gazeti la Washington
Post.
Mke wa Donald Trump ajitokeza kumtetea
Baada ya kufichuliwa kwa ukanda huo, viongozi
wengi wakuu wa chama cha Republican walijitenga
na Bw Trump ambayo yamezua utata.
Kwenye video hiyo, Bw Bush anasikika akicheka
baada ya matamshi ya Bw Trump.
Billy Bush, 45, ambaye ni mpwa wa rais wa zamani
George H W Bush, alikuwa awali amesimamishwa
kazi baada ya kufichuliwa kwa video hiyo.
Trump 'aliwapapasa wanawake kama pweza'
Amekuwa mtangazaji wa kipindi cha Today kwa
miezi miwili pekee.
"Ingawa alikuwa mgeni tu katika waandaaji wa
kipindi cha Today, amekuwa na NBC kwa muda
mrefu. Tunamtakia kila la heri," shirika la NBC
limesema kupitia taarifa.
Mke wa Donald Trump, Melania, amemshutumu Bw
Bush akisema alimchochea mumewe kusema
mambo mabaya kuwahusu wanawake.
Bw Bush mwenyewe aliomba radhi tarehe 7
Oktoba akisema binafsi pia aliaibishwa na tabia
yake alipokuwa akifanya mahojiano hayo.f
No comments:
Post a Comment