Tuesday, October 18, 2016

Diamond na Harmonize washinda tuzo Marekani

Afrika Mashariki imekuwa na furaha kubwa wikendi
kwenye tuzo za kila mwaka za Jarida la mziki
Afrika, maarufu kama Afrimma Awards baada ya
wasanii wa Kenya na Tanzania kuzoa tuzo tofauti
kwenye hafla iliyofanyika Marekani wikendi.
Imekuwa ni ushindi mkubwa kwa Wasanii wa lebo
ya Wasafi kutoka Tanzania, Diamond Platnumz na
Harmonize walioibuka mabingwa kwenye vitengo
vyao.
Diamond alimshinda Mtanzania mwenzake, Ali Kiba
katika kitengo cha mwanamuziki bora wa kiume
Afrika Mashariki.
Harmonize, anayezidi kuvuma kwa wimbo wake wa
'Inde' aliomujmuisha Dully Sykes, akitunukiwa tuzo
ya Msanii mpya wa mwaka.
Diamond Platinumz: Usitosheke kuvuma
nyumbani pekee
Hata hivyo Diamond hakuweza kuhifadhi taji lake
la msanii bora wa mwaka aliloshinda mwaka wa
2015 kwani tuzo hiyo ilikwenda kwa Mnigeria
Falvour.
Kwa upande mwingine, Kenya ilipata tuzo tatu
kupitia Msanii wa nyimbo za injili, Willy Paul,
aliyeshinda kitengo cha msanii bora wa injili nalo
kundi la Sauti Soul likapewa tuzo ya kundi bora la
mwaka.
Mwanamuziki wa kike, Akothee, aliondoka na taji la
mwimbaji bora wa kike licha ya mashabiki kutishia
kutompigia kura.f

No comments:

Post a Comment