zisizo na rubani Rwanda
Maeneo mengi ya Rwanda yana milima na
misitu hivyo huwa vigumu kusafiri kwa kutumia
barabara
Huduma ya kusafirisha damu na vifaa vingine
vya kimatibabu kwa kutumia ndege zisizo na
rubani, inazinduliwa leo nchini Rwanda.
Huduma hiyo ni ya kwanza ya aina yake
duniani.
Ndege zisizo na marubani zitakuwa zikipaa moja
kwa moja hadi eneo ambalo damu inahiajika
nchini Rwanda, na kisha kurejea kituoni.
Badala ya kutua ndipo ziwasilishe kifurushi
chenye damu, kifurushi hicho kitarushwa ardhini
salama kwa kutumia mwavuli au parachuti.
Teknolojia hiyo inaleta matumaini ya kuwasilisha
damu haraka na kwa njia salama ukilinganisha
na awali ambayo njia ya kutegemewa pekee
ilikuwa barabara, nyingi ambazo ambazo hali
yake ni mbaya.
Vifurushi vitakuwa vikirushwa ardhini kwa
kutumia mwavuli au parachuti. Ndege
hazitahitaji kutua.
Kampuni ya Marekani ya Zipline ndiyo
itakayoendesha mradi huo.
Wanaofanya kazi katika kampuni hiyo ni
wahandisi ambao awali walifanya kazi katika
kampuni maarufu za kiteknolojia kama vile
Space X, Google, na Lockheed Martin..
Mwanzoni, ndege hizo zitatumiwa kusafirisha
damu, maji ya damu na dutu inayogandisha
kioevu.
Ndege hizo zinaweza kuruka na kupaa zikiwa
futi 500 (mita 152) juu ya ardhi kuzuia
kugongana na ndege kubwa za kawaida
zinazobeba abiria na mizigo.
Ndege hizo zitakuwa zinahudumu eneo la umbali
wa hadi kilomita 150 (maili 93), ingawa zina
uwezo wa kwenda umbali maradufu ya umbali
huo.
Ndege hizo za Zipline zikirushwa angani kutoka
kwenye kambi iliyopo karibu na mji wa Kigali
Ndege hizo zinatumia nguvu za umeme kutoka
kwenye betri na hutumia teknolojia ya GPS
kuziongoza kufika maeneo yanayotakikana.
Zitakuwa zikituma maeleo kwa wahudumu
kwenye kambi ya ndege hizo na pia wahudumu
wasimamizi wa safari za ndege Rwanda kwa
kutumia teknolojia ya mawasiliano ya simu.
Kwa kuanza, ndege 15 zitakuwa zikifanya kazi.
Ndege hizo, ambazo kwa kifupi zinafahamika
kama 'Zip', zina uwezo wa kupitia hata kwenye
upepo wa kasi ya kilomita 30 kwa saa (19mph)
au mvua ndogo hali ikibidi.
Wakati wa kufanyiwa majaribio kwa teknolojia
hiyo, jeshi la Rwanda lilionesha kuvutiwa
Zipline italipwa na idara ya afya ya Rwanda kwa
kila safari itakayofanywa na ndege hizo.
Kampuni hiyo inasema gharama ya kila safari
moja ni karibu sawa na ya kutumia pikipiki au
ambiulensi.
Wahudumu wa afya wanasema kuomba huduma
ya Zipline kwa kutumia ujumbe mfupi
Ndege zisizo na rubani tayari zimetumiwa kwa
shughuli za kibinadamu kwingineko Afrika,
ikiwemo kusafirisha sampuli za damu na kinyesi
nchini Madagascar. Aidha, kuna mradi wa
Shirika la Msalaba Mwekundu unaotumiwa
kufuatilia shughuli kambi ya wakimbizi Uganda.
Lakini baadhi ya wafanyakazi wa mashirika ya
misaada wanasema ndege hizo mara nyingi
huwa hazifai.
"Upende usipende, ndege hizo mara nyingi
hudhaniwa kuwa ndege za kutekeleza
mashambulio au kufanya ujasusi," mmoja wa
wahudumu waliofanya kazi DR Congo aliambia
watafiti wa wakfu mmoja kutoka Uswizi.
Ingawa jeshi la Rwanda limeonekana kuvutiwa
na kazi ya Zipline, waziri wa teknolojia, habari
na mawasiliano Rwanda amesema hakuna
mipango yoyote kwa sasa kwa jeshi kutumia
teknolojia hiyo.
No comments:
Post a Comment