Wednesday, October 19, 2016

Chombo cha anga za juu cha Ulaya kutua Mars

Chombo cha anga za juu cha Ulaya Schiaparelli
kimefanikiwa kujitenga na "chombo mama" angani
na kwa sasa kinaelekea kwenye sayari ya Mars.
Chombo hicho kinatarajiwa kujaribu kutua kwenye
sayari hiyo Jumatano.
Chombo hicho cha uzani wa kilo 577 kilifanikiwa
kujitenganisha na chombo mama Jumapili saa
14:42 GMT (saa kumi na moja jioni saa za Afrika
Mashariki).
Mpango wa kupeleka watu wakaishi Mars
Mpango wa Marekani kupeleka watu Mars
Chombo hicho kitakuwa na muda wa chini ya
dakika sita kupunguza kasi yake ya kilomita
21,000 kwa saa kiasi cha kukiwezesha kutua
salama kwenye sayari hiyo.
Schiaparelli ni kifaa cha kufanyia majaribio
teknolojia, na lengo kuu ni kudhihirisha uwezo wa
Shirika la Anga za Juu la Ulaya (ESA) kutua katika
sayari hiyo.
Jaribio la awali la shirika hilo kutua katika sayari
hiyo lilifanyika mwaka 2003, kwa kutumia chombo
cha Uingereza cha Beagle-2.
Chombo hicho kilifanikiwa kutua salama lakini
kikashindwa kufungua mitambo yake ya kawi ya
jua vyema na hivyo mawasiliano yakakatika.
Chombo hicho kikifanikiwa kutua salama,
kitatumiwa kufanya uchunguzi kwenye sayari hiyo.

No comments:

Post a Comment