Thursday, September 22, 2016

Progamu ya Windows 10 lawamani






Kampuni ya Microsoft imeshtumiwa na kundi la
haki za wateja la Consumer Rights dhidi ya
programu yake ya Windows 10.
Kundi hilo limesema limepokea mamia ya
malalamishi kuhusiana na uboreshaji wa
programu hiyo .
Watumiaji wa programu hiyo wanalazimika
kulipia komputa zao ili zirekebishwa kutokana na
faili kupotea.
Hatahivyo Microsoft ilitetea programu hiyo ya
Windows 10 na kusisitiza kuwa imekuwa ikitoa
usaidizi kupitia mtandaoni na vilevile kwa simu.
Imeongezea kwamba itawasaidia watu kupata
programu yenye manufaa na yenye usalama
dhabiti, kulingana na msemaji wa kampuni hiyo.
Kundi hio limesema watumiaji wamekuwa
wakilalamikia ujumbe uliokuwa ukijitokeza
kwenye tarakilishi na simu zao kila mara,
kuwahimiza kuboresha programu hiyo mbali na
programu hiyo ya Windows 10 kujiweka yenyewe
bila idhini ya mtumiaji.
Pia kumekuwa na malalamiko kuhusiana na
huduma mbaya kwa wateja wake,pale
wanapohitaji msaada kutoka kwa kampuni hiyo.
Programu hiyo ya windows 10 ilizinduliwa mwezi
Julai mwaka 2015, na hutumika katika
tarakilishi,simu aina ya smartphone, na vifaa vya
kusikilizia sauti vya HoloLens.

1 comment: