Tuesday, August 9, 2016

SERIKALI IMESEMA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOJIUNGA NA VYUO VIKUU BILA KUWA NA SIFA YATATANGAZWA MWEZI UJAO

Serikali imesema majina ya wanafunzi waliojiunga na vyuo vikuu bila kuwa na sifa yatatangazwa mwezi ujao na kuondolewa masomoni, baada ya uhakiki wake kukaribia kukamilika. Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, amesema ameshawaagiza watendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) kufanyia kazi suala hilo. Ili kuwabaini wanafunzi wote wasio na sifa, waziri huyo alisema tayari tume hiyo imeanza uhakiki vyeti vya wanafunzi wote waliopo vyuoni.

Unauchukuliaje uamuzi huu, uko SAHIHI au WAMECHEMSHA?

No comments:

Post a Comment