POGBA RASMI OT
Paul Pogba amesema "huu ni wakati muafaka kurejea Old Trafford" baada ya kukamilisha uhamisho uliovunja rekodi ya dunia wa pauni milioni 89 kwenda Manchester United. Kiungo huyo, 23, amerejea Manchester miaka minne baada ya kuondoka na kwenda Juventus mwaka 2012. Pogba ambaye amesaini mkataba wa miaka mitano amesema: "Hii ni klabu inayonifaa kuweza kufikia mafanikio ninayotaka." Meneja Jose Mourinho amesema mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa anaweza kuwa "roho ya klabu hiyo" kwa muongo ujao. United watawalipa Juventus euro milioni 105 pamoja na bakshishi ya euro milioni 5. Ada hiyo inapita ile iliyolipwa kumsajili Gareth Bale ya pauni milioni 85 kwenda Real Madrid kutoka Spurs mwaka 2013 ambayo ilikuwa ndio rekodi ya dunia. Picha kwa hisani ya tovuti ya Manchester United
No comments:
Post a Comment