Monday, August 29, 2016

Udhaifu mkubwa wagunduliwa kwenye simu za iPhone





Mfumo wa Apple wa utendaji wa iOS umegundulika ambao utawezesha kupachikwa kwenye kifaa cha uchunguzi kukiwezesha kubofya kwenye kiunganishi.
Uvumbuzi huo ulifanyika baada ya wakili anayetetea haki za kibinadamu kutoa taarifa kwa watafiti wa masuala ya usalama kuhusu jumbe alizozipata bila kutarajia.
Waligundua taarifa nyingine tatu za awali zisizofahamika zilizovuja kutoka kwa mfumo wa Apple .
tangu wakati huo Apple imetoa taarifa ya kuelezea tatizo hilo na namna linavyoshughulikiwa na kampuni hiyo.
Makampuni mawili ya usalama yaliyohusika , Citizen Lab na Lookout, yamesema yamehifadhi taarifa hizo za uvumbuzi hadi suala hilo litakapopatiwa ufumbuzi.
Kampuni ya Citizen Lab inasema , simu yake ya iPhone 6 ingekuwa ''imefunguliwa'' , ikimaanisha mfumo mwingine ambao haukuidhinishwa ungelikuwa umewekwa kwenye simu yake.
"Na kama simu yake ingeathiriwa , ingekuwa kifaa cha upelelezi cha digitali ndani ya mfuko wake wa nguo, yenye uwezo wa kung'amua taarifa kwa kutumia kamera na kipaza sauti cha simu kurekodi simu zake za WhatsApp na Viber , kuingia kwenye jumbe alizotuma kwa simu na kuweza kumfuatilia kote anakoenda," ilisema kampuni ya Citizen Lab.
"Hatuna taarifa zozote za matukio ya aina hii ya iPhone suala linalofanya tukio hili kuwa la nadra ."
Watafiti wanasema wanaamini mfumo huu wa uchunguzi unaohusisha spyware ulibuniwa na kampuni ya NSO Group, ya Israel ya ''vita vya mitandaoni"

Wednesday, August 24, 2016

Belle 9 amejiunga na kambi ya WCB, tayari kaanza kufanya mazoezi na Diamond


Baada ya vocalist, Rich Mavoko kusaini WCB ya Diamond, huwenda msanii wa muziki wa R&B kutoka Morogoro, Belle 9 na yeye akasaini ndani ya label hiyo.
Muimbaji huyo anayefanya vizuri na wimbo ‘Bugger Movie Selfie’ ameonekana akifanya mazoezi ya bendi ya Diamond katika ofisi za WCB.
Kwa mujibu wa kipindi cha Planet Bongo cha EATV, Belle pamoja na Diamond wameonekana wakiimba wimbo ‘Mdogo Mdogo’ kwa pamoja huku wakicheza.
Hatua hiyo imefufua matumaini mapya kwa mashabiki wa kumuziki kuona huweza WCB ikamsaini msanii hiyo kama ilivyofanya kwa Rich Mavoko.
Kwa sasa label ya WCB ina wasanii wanne, Harmonize, Rich Mavoko, Raymond aka Rayvany pamoja Queen

Fiesta Show Mwanza 2016 Walio Fanya Good.


Fiesta Show Mwanza 2016 Walio Fanya Good.


WA KAGERA MULEBA TWENDE SAWA,,,,,,,FIESTA KAGERA IMOO!Nunua tiketi yako kwa TigoPesa kwa Sh 4000TU.Piga *150*01# chagua TUMA PESA kisha TUMA KWA NAMBA YA SIMU (namba ya mpokeaji ingiza 0678 888 888).Hakikisha unasalio la Sh 4500 katika akaunti ya TigoPesa


Tuesday, August 9, 2016

SERIKALI IMESEMA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOJIUNGA NA VYUO VIKUU BILA KUWA NA SIFA YATATANGAZWA MWEZI UJAO

Serikali imesema majina ya wanafunzi waliojiunga na vyuo vikuu bila kuwa na sifa yatatangazwa mwezi ujao na kuondolewa masomoni, baada ya uhakiki wake kukaribia kukamilika. Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, amesema ameshawaagiza watendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) kufanyia kazi suala hilo. Ili kuwabaini wanafunzi wote wasio na sifa, waziri huyo alisema tayari tume hiyo imeanza uhakiki vyeti vya wanafunzi wote waliopo vyuoni.

Unauchukuliaje uamuzi huu, uko SAHIHI au WAMECHEMSHA?

DONDOO ZA SOKA ULAYA

POGBA RASMI OT
Paul Pogba amesema "huu ni wakati muafaka kurejea Old Trafford" baada ya kukamilisha uhamisho uliovunja rekodi ya dunia wa pauni milioni 89 kwenda Manchester United. Kiungo huyo, 23, amerejea Manchester miaka minne baada ya kuondoka na kwenda Juventus mwaka 2012. Pogba ambaye amesaini mkataba wa miaka mitano amesema: "Hii ni klabu inayonifaa kuweza kufikia mafanikio ninayotaka." Meneja Jose Mourinho amesema mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa anaweza kuwa "roho ya klabu hiyo" kwa muongo ujao. United watawalipa Juventus euro milioni 105 pamoja na bakshishi ya euro milioni 5. Ada hiyo inapita ile iliyolipwa kumsajili Gareth Bale ya pauni milioni 85 kwenda Real Madrid kutoka Spurs mwaka 2013 ambayo ilikuwa ndio rekodi ya dunia. Picha kwa hisani ya tovuti ya Manchester United